My website
Email : info@applevalleyhealth.ac.tz Call : 0764222999

Apple Valley Institute of Health Science And Technology

healthy practice, healthy care

KURIPOTI CHUONI 03/10/2022

APPLE VALLEY INSTITUTE OF HEALTH SCIENCE AND TECHNOLOGY IMEDHAMINI MATEMBEZI NA MBIO MAALUM (KM 5) - KIGAMBONI YALIYOANDALIWA NA APPLE VALLEY POLYCLINIC

APPLE VALLEY INSTITUTE OF HEALTH SCIENCE AND TECHNOLOGY IMEDHAMINI MATEMBEZI NA MBIO MAALUM (KM 5) - KIGAMBONI  YALIYOANDALIWA NA APPLE VALLEY POLYCLINIC

 

Matembezi na Mbio Maalum za urefu wa Kilomita 5 Wilayani Kigamboni yaliyoandaliwa na Apple Valley Polyclinic chini ya Muwekezaji na Mkurugenzi Mkuu wake Dkt. Evans Rweikiza, yamefanyika kikamilifu leo tarehe 05, Machi 2022.

Matembezi hayo yaliambatana na utoaji wa huduma za kijamii kukiwa na zoezi la Uchangiaji wa Huduma, Utoaji Chanjo ya UVIKO-19, Kupima Afya kwa magonjwa ya Blood pressure, Ugonjwa wa Kisukari na HIV.

Aidha Katika utoaji huduma hizo, Wananchi wakazi wa maeneo mbalimbali ya Kigamboni waliojotokeza kushiriki, wamemshukuru na kumpongeza Bw. Dkt. Rweikiza kwa kuandaa na kufanikisha jambo hili kubwa na kumuomba ikiwezekana lisiihie kwa leo tuu bali liwe jambo la muendelezo kwani ji lenye tija na manufaa makubwa katika kujali na kuwakumbusha watu wengi kuzingatia Afya zao.

Katika matembezi hayo, Mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni aliyewakilishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kigamboni Ndg. Greyson Mwinkola.

#MazoeziNiAfyaJaliAfyaYakoJipende

KaziIendelee